Advertising

FAHAMU MADHARA YA CHIPS NA SODA

CHIPS

Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree. 
Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija 
Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini. Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana tunapokula vyakula vyingi vyenye mafuta mengi hutupelekea kuongeza unene na uzito.

Unene huwa ni chanzo cha magonjwa
mengi ,Kwani (High Blood pressure) hutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini ambayo hupelekea mirija ya kusafirisha damu kuwa na mafuta. Hii husababisha njia ya kupitia damu kuwa nyembamba hivyo kusababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini kama inavyotakiwa. Nguvu hii ya ziada huongeza au kupunguza mapigo ya moyo. Mapigo ya moyo yanapoongezeka sana ni hatari na yanapo pungua sana pia ni hatari. 

Hivyo basi ni vizuri kwa watumiaji wa chipsi kujitahidi kutumia kwa kiasi kidogo au kuacha kabisa vile vile mazoezi pia ni muhimu ili kupunguza mrundikano wa mafduta katika mwili.
Pia inasemekana kuwa wanasayansi wamegundua kuwa chipsi husababisha kukuza hips hivyo kwa wanaume wengi hawatapenda kuwa katika hali hiyo, hivyo ni muhimu kujiepusha na pia isije ikawa kichocheo kwa wanawake kutumia sana ili kukuza sehemu hizo za maumbile bali wapunguze kutumia chipsi pamoja na kufanya mazoezi ili kuweka mwili katika hali ya kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.pia ulaji wa chips kupita kiasi husababisha wanaume na wanawake kuzeeka mapema.
SODA
Moja ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi ni pamoja na soda. Matangazo mengi ya biashara yanafanyika kutangaza kinywaji cha soda na kuonesha kuwa ni kinywaji ambacho hakina madhara kabisa kwa mtumiaji. Kwa matangazo hayo na kampeni hizo, familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii.
Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda kama vile ni sumu, lakini watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe, hata kwa wanywa soda ilipaswa kutolewa pia.
Utafiti unaonesha kuwa soda, pamoja na vikorombwezo vingine, huwekwa sukari nyingi kiasi kisichopungua vijiko sita katika chupa moja. Kiwango hicho cha sukari ni kingi zaidi ya mara tano ya kile kinachoruhusiwa kwa mtu kutumia kwa siku. Na madhara ya sukari mwilini ni mengi, yakiwemo ya kudhoofisha kinga ya mwili na viungo kwenye sehemu za maungio na pia huongeza uzito wa mwili.
Ukitaka kujua soda ina madhara kiafya, fanya utafiti binafsi na utagundua haya ninayoyaandika. Kunywa soda zisizopungua tatu kwa muda mfupi, kisha lala usiku kama kawaida halafu wakati wa kuamka asubuhi, usikilize mwili wako. Utaamka ukiwa na maumivu mwili mzima, utajihisi uchovu, hasa sehemu za maungio, mfano wa mtu aliyefanya mazoezi mazito au kazi nzito siku iliyopita. Hiyo ni kutokana na kuingiza kiwango kingi cha sukari mwilini.
watafiti kutoka shule ya tafiti ya harvard wameeleza athari inayoweza kutokea na kuathiri figo kwa  wanawake. watafiti hao wameeleza kuwa madhara hayo yanaweza kuwapata wanawake hasa wanapo kunywa soda zaidi ya mara mbili kwa siku. kwani figo huanza kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi wa kawaida. pia wamevihusisha vyakula vyenye sukari nyingi kuwa chanzo cha madhara katika figo. 
FAHAMU MADHARA YA CHIPS NA SODA FAHAMU MADHARA YA CHIPS NA SODA Reviewed by Unknown on 11:03 AM Rating: 5

No comments:

Events

Powered by Blogger.