KAMA ULIKATALIWA AU ULIFELI, USIKATE TAMAA.
KAMA ULIKATALIWA AU ULIFELI, USIKATE TAMAA.
Jan Koum, si jina geni sana masikioni mwa wafuatiliaji wa habari za ulimwengu. Lakini, historia yake yawezakuwa ngeni kwa wengi. Kijana huyu, aliyelelewa nchini Ukraine, akiwa na umri wa miaka 16 tu, mwanzoni mwa miaka ya tisini (1990's) ndipo aliingia nchini Marekani pamoja na wazazi wake, wakiwa kama wahamiaji.
Kipato cha familia yao kilikidhi mahitaji ya tumbo tu, na zaidi ya hapo. Yeye mwenyewe aliposhindwa kuhitimu "High school", alikimbilia kujiunga na chuo cha San Jose state university, lakini napo "alipigwa chini".
Mwaka 2009 maombi yake ya kufanya kazi katika kampuni ya Facebook yalikataliwa. Ikawa ni balaa juu ya mkosi, lakini hakukata tamaa kwakuwa alikiamini kipaji chake. Mwaka huohuo, alibuni na kutengeneza application ya " WhatsApp" iliyoushangaza ulimwengu kwa kujizolea zaidi ya watumiaji milioni 450, huku watumiaji wa uhakika kwa kila siku wakifikia milioni moja.
Miaka minne baadaye, yaani, 2014. Wamiliki wa mtandao wa Facebook, walewale waliomkataa Jan Koum, mwaka 2009, walimfikia kijana huyo na kumpa offer ya kuinunua WhatsApp yake kwa dola za kimarekani bilioni 19. Pamoja na kuinunua WhatsApp kwa bei hiyo, bado Jan Koum alibakiwa na hisa asilimia 14 za umiliki.
MAZINGATIO: Bila ya kujali magumu unayopitia, vikwazo vinavyokuzibia njia, kushindwa au kukataliwa. Kumbuka, endapo hutakata tamaa na kuamua kutumia kipaji chako katika njia mbadala, basi daima iko kesho yenye mafanikio makubwa. Kesho ambayo utatuzwa kwa thamani kubwa na walewale waliokupuuza na kukukataa.
KAMA ULIKATALIWA AU ULIFELI, USIKATE TAMAA.
Reviewed by Unknown
on
7:42 PM
Rating:
No comments: