Advertising

Kilimo Bora cha Nyanya; Maandalizi Ya Mbegu, Shamba Na Upandaji Wa Miche, Magonjwa

Kilimo cha Nyanya

 Image result for kilimo cha kisasa cha nyanya

KARIBU KATIKA KILIMO CHA NYANYA
NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta, au waswahili wanaimuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..
WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA

DAWA ZA KUTUMIA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yle moth kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)

2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Arysta Life Science inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana

AGRONOMY YA NYANYA
AINA
Ziko nyingi kama fupi kiasi (Semi Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA

A; Semi-determinent
1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-

B; Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU
AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA
C; AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima

MAZINGIRA
i. Joto la kadri 20-35 degree sentigrade

ii. UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo

iii. NAFASI YA KUPANDA
-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapnada double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE
-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA

Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)
Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)
KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 30-50 kwa hybrid (F1) . Ghrama za kutosha eka moja kwa OPV variety ni tsh 100,000-180,000, na kwa Hybrid (F1) Gharama ni kati ya tsh 200,000-400,000 kutegemea na aina yenyewe ya mbegu.

UPANDAJI
Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowte utakao, na kisha chora vimefereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dodondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia mwaji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.
Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)
MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.
ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.
MAMBO YA KUFANYA SHAMBANI
Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung’oa miche, na sahamba mama pia liwe limemwagiwa vya kutosha
-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)
Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo paada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji
BAADA YA KUPANDIKIZA
Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani
Dawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao
Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, UREA, Yarra miller winner, au Hata NPK,
Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitumba vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) kama vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix
WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU
Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipingwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana sa 6 hadi sa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shape less
MATUNDA YAKIJA
Ni muhimu kuzungusha chini katika mizii mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking
WADUDU
Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)
Magonjwa
Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)
MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 120 HADI 150 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA

MAVUNO
Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 65
SOKO
Nyanya yenye bei nzuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000
Gharama za kuhudumu shamba la Nyanya kwa eka 1 ni takribani 2.5 hadi 3.5 Milioni ( Gharama kubwa ipo, katika mbegu hasa kama ni hybrid (F1), mbolea, maji (Pump), Vibarua (wakati wa kupanda na kupalilia) na madawa ya kuzuia wadudu na kutibu magonjwa.
Kilimo Bora cha Nyanya; Maandalizi Ya Mbegu, Shamba Na Upandaji Wa Miche, Magonjwa Kilimo Bora cha Nyanya; Maandalizi Ya Mbegu, Shamba Na Upandaji Wa Miche, Magonjwa Reviewed by Unknown on 2:12 PM Rating: 5

No comments:

Events

Powered by Blogger.