Advertising

Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili Vyama Vitatu

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi ametangaza kuvifutia usajili vyama vitatu baada ya kubainika kukiuka sheria ya usajili wa vyama.

Vyama hivyo ni pamoja na CHAUSTA kilichopata usajili wa kudumu tarehe 5 Novemba 2001, The African Progressive Party of Tanzania ( APPT-Maendeleo) kilichopata usajili wa kudumu terehe 4 Machi 2003 na Chama cha Jahazi Asilia kilichopata usajili wa kudumu tarehe 17 Novemba 2004.

Jaji Mutungi amesema kuwa mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo umetokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika kuanzia tarehe 26 Juni hadi 26 Julai 2016.

Amesema katika zoezi hilo uhakiki ulibaini kuwa vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, na kwamba kila chama kilipewa ya nia ya msajili kufuta usajili wake, lakini vikashindwa kutoa utetezi wa kuridhisha ili visifutiwe usajili.

Kufuatia uamuzi huo, Msajili amewataka waliokuwa wanachama wote wa vyama hivyo kutojiuhusisha na shughuli yoyote kwa majina ya vyama hivyo, na kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria, huku akiviasa vyama vingine kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria.
Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili Vyama Vitatu Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili Vyama Vitatu Reviewed by Unknown on 8:29 PM Rating: 5

No comments:

Events

Powered by Blogger.