Advertising

NI NANI ANAYETHUBUTU KUKATIZA NDOTO ZAKO? ACHANA NAYE, SONGA MBELE!

NI NANI ANAYETHUBUTU KUKATIZA NDOTO ZAKO? ACHANA NAYE, SONGA MBELE!
Image result for famous
1. STEVE JOBS
Akiwa na miaka 30 aliachwa amechanganyikiwa na mwenye huzuni baada ya kuondolewa kikatili kwenye kampuni aliyokuwa ameianzisha. Baadaye alisimama imara na leo mamilioni ya binadamu wanajifunza kutoka kwenye mafanikio yake.
2. WALT DISNEY
Alifukuzwa kutoka kwenye gazeti kwa kile kilichoitwa “kukosa maono” na “kukosa mawazo ya msingi”, baadaye sote tunajua amekuja kuwa “KING OF THE CARTOON” Movies and everything. Tajiri wa kutupwa.
3. ALBERT EINSTEIN
Hakuwa na uwezo wa kuongea hadi alipofikisha miaka minne na walimu wake walimchukulia kama mtu asiyeweza kubeba mambo mengi. Tuongeavyo hapa huyu ndiye Mwanafizikia aliyesaidia kuibadilisha dunia.
4. OPRAH WINFREY
Aliondolewa kazini kama Mtangazaji kwa sababu wamiliki waliona “hawezi kufaa kwenye TELEVISHENI”, leo yeye ndiye mmoja wa watangazaji tajiri na mwanamke wa kupigiwa mfano duniani.
5. MICHAEL JORDAN
Alipoondolewa kutoka kwenye timu yake ya mpira kwa kukosa uwezo, alienda nyumbani kwao akajifungia chumbani na kuanza kulia kwa kukatizwa ndoto zake. Baadaye alijipanga kivyake na leo yeye ndiye mchezaji wa mpira wa kikapu wa karne.
6. THE BEATLES
Waimbaji hawa walikataliwa na studio iitwayo DECCA kwa kile kilichoitwa “hawaonekani kama wanamuziki wataokuja kufanikiwa kwenye muziki”. Walijipanga kivyao na baadaye wakaja kuwa bendi inayovunja rekodi kubwa kubwa duniani, ikiwamo ya mauzo ya kazi zao za muziki.
Wakati unakaribia mwaka 2017 acha kukata tamaa, weka mipango sawa na songa mbele.
MWANADAMU AKIKWAMBIA HUWEZI WEWE MWAMBIE MUNGU ALIYENIUMBA NDIYE ANAJUA
NI NANI ANAYETHUBUTU KUKATIZA NDOTO ZAKO? ACHANA NAYE, SONGA MBELE! NI NANI ANAYETHUBUTU KUKATIZA NDOTO ZAKO? ACHANA NAYE, SONGA MBELE! Reviewed by Unknown on 9:14 AM Rating: 5

No comments:

Events

Powered by Blogger.