UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, SABABU NA TIBA.
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, SABABU NA TIBA.
Upungufu wa nguvu za kiume ni ugonjwa ambao mwanaume hushindwa
kusimamisha uume na pia kushindwa kuendelea kubaki imara wakati wa tendo la
ndoa. Uume kusimama hutokea pale damu
inapoingia katika tishu zilizo kama sponji na kuendelea kubaki ndani yake
wakati wa tendo la ndoa.Hii hutokea kama matokeo ya mhemko kabla ya tendo la
ndoa, ambapo taarifa hupelekwa kwenye ubongo na hatimaye taarifa hutumwa katika
mishipa fahamu iliyo katika
uume.
uume.
Sababu zinazosabisha tatizo hili
zaweza kugawanywa kama ifuatavyo:-
a) Hitilafu
katika ogani za mwili (Organic causes)
Hitilafu hizi
ambazo zinatambulika zaidi ni kama magonjwa ya moyo na kisukari,upungufu wa
homoni mwilini (kitaalam kama hypogonadism)
,maudhi yasiyotakiwa ya dawa mbalimbali(side
effects), pia magonjwa ya mishipa ya fahamu yanayoweza kusababishwa na
kuumia au kufanyiwa operesheni ya tezi dume.
Pia zifuatazo ni
sababu nyingine katika kundi hili
- Kuziba kwa mishipa ya damu.
- Kiwango kikubwa cha lehemu katika damu.
- Unene (Obesity).
- Kukosa usingizi.
- Unywaji pombe kupindukia na madawa ya kulevya.
- Utumiaji wa tumbaku.
- Kuumia kwa uti wa mgongo.
- Magonjwa ya mmeng’enyo.
b)Matatizo
ya kisailolojia
- Sononi, wasiwasi na hata magonjwa mengine yanayoathiri afya ya akili.
- Msongo wa mawazo.
- Matatizo ya uhusiano ambayo hupelekea msongo wa mawazo, hata mawasiliano yaliyo duni.
c) Mchanganyiko
wa hitilafu katika Ogani na Saikolojia kwa pamoja.
Tunavyoozeeka
tatizo hili laweza kuongezeka, ingawa siyo hali ya kawaida mtu anapozeeka.
Wazee ni kundi ambalo hutumia dawa za matatizo mbalimbali kwa wingi. Kwa hiyo
tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume linapotokea mara nyingi huashiria
hali ya kiafya isiyo ya kawaida au kusabishwa na aina fulani za dawa atumiazo
mgonjwa. Mara nyingi hutokea kwa wale walio na miaka 60 na kuendelea. Hata
hivyo vijana huweza pia kupata tatizo hili.
Pia wanaoweza
kupata tatizo hili ni kama:-
- Wenye matatizo ya kiafya, kama ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa moyo.
- Wenye kuendesha baiskeli kwa muda mrefu, uendeshaji wa baiskeli bila kutumia vifaa maalum waweza kusababisha kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu na kuathiri mzunguko wa damu katika uume.
- Watumiaji wa dawa za kulevya pamoja na pombe, hususan watumiaji wa muda mrefu na unywaji pombe kupindukia.
- Wenye msongo wa mawazo,sononi na wasiwasi
- Wenye kutumia aina mbalimbali za dawa.
- Waliojeruhiwa, hususan mishipa ya fahamu husika.
- Wenye uzito mkubwa, hasa walio wanene.
- Wenye kutumia tumbaku, ambayo huathiri mtiririko wa damu katika mishipa ya uume ya ateri na veini.
Matatizo yenye kujitokeza ugonjwa
usipotibiwa
- Kutoridhika katika uhusiano.
- Msongo wa mawazo na wasiwasi.
- Sononi.
- Kujisikia vibaya mbele ya jamii na kutokujiamini.
- Matatizo ya uhusiano au kuvunjika kwa uhusiano.
- Kutokuwa na uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke.
Endapo tatizo hili litajitokeza,
usikimbilie kuanza kutumia dawa, au kununua dawa katika famasi bila ushauri wa
daktari. Dawa hazitakuwa na msaada
endapo chanzo cha tatizo hakijagundulika. Pia matumizi ya dawa yanaweza
kukuletea athari nyingine kiafya, kama uchunguzi haukufanyika kwanza.
Jiandae kumwona daktari wako, kwa kukusanya taarifa mbalimbali kama
dalili za ugonjwa ulizo nazo, listi ya dawa unazotumia, uwe na taarifa muhimu
za kukuhusu, ni vyema ukienda na mwenzi wako kwa kuwa atakuwa msaada kwa yale
uliyosahau na andaa maswali utakayomuuliza daktari wako.
Vipimo mbalimbali vyaweza kutumika ili kugundua sababu ya ugonjwa.
Vipimo hivi hujumuisha vile vya kuchunguza mzunguko wa damu katika uume, pia
kipimo maalum cha kuvaa nyakati za usiku kuchunguza mara ambazo uume unasimama
ukiwa umelala, na vile vya kuchunguza viwango vya homoni mwilini.
Pia historia ya mgonjwa itamwezesha daktari kuweza kugundua tatizo la
mgonjwa akishirikisha na vipimo mbalimbali tulivyovitaja hapo awali
Daktari ana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa unapata
tiba sahihi kulingana na kisababishi cha ugonjwa na kinachofanya hali kuwa
mbaya kama tulivyoona awali.
Kulingana na sababu inayosabisha ugonjwa wa upungufu wa
nguvu za kiume, unaweza kutibiwa kwa njia mbalimbali. Daktari wako na mfamasia
watakuelezea faida na hasara ya kutumia tiba husika na watajali zaidi uamuzi
wako. Pia mawazo ya mwenzi wako yatasaidia ili uweze kupata tiba iliyo sahihi.
Dawa za kumeza zinatumika sana katika kutibu upungufu wa
nguvu za kiume na zimeonyesha mafanikio makubwa. Dawa hizi ni kama zifuatazo:-
a) Dawa
zinazoongeza mzunguko wa damu katika uume,
- Tadalafil(Sialis)
- Sildenafil (Viagra)
- Verdenafil ( Levitra)
- Avanafil (Stendra)
Tahadhari
Chukua tahadhari kabla ya kutumia dawa yeyote kutibu
nguvu za kiume, hata kama ni dawa za kienyeji au zile zinazonunuliwa bila ya
kuandikwa na daktari. Wasiliana na mfamasia kwa ushauri zaidi.
Dawa zitumiwapo ovyo zinaweza zisikusaidie kutatua
tatizo na zaweza kuwa hatari kama:-
- Unatumia dawa zenye nitrate-ambazo huandikiwa wagonjwa wenye maumivu ya kifua (angina), kwa mfano Nitroglycerin,Isosorbide mononitrate na isosorbide dinitrate.
- Unameza dawa za kusaidia mtiririko wa damu (anticoagulant) au dawa za shinikizo la juu la damu.
- Una tatizo la moyo au moyo kushindwa kufanya kazi.
- Una ugonjwa wa kiharusi au uliwahi kupata kiharusi.
b) Dawa
za homoni.
Dawa kama
testosterone yaweza kutumika kwa wanaume wenye upungufu wa homoni hiyo. Kwa
wale wenye upungufu wa homoni dawa hii inaweza kuwa tiba ya kwanza
Upasuaji waweza kufanyika
endapo mishipa ya damu ya uume itakuwa imeziba na kusababisha upungufu wa nguvu
za kiume.
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, SABABU NA TIBA.
Reviewed by Unknown
on
12:40 PM
Rating:
No comments: